NOVENA HII IMEANZA IJUMAA TAREHE 31 NA ITAMALIZIKA TAR 8 JUNI SIKU YA JUMAMOSI
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU
Mpangilio wa sala na nyimbo kwa
siku zote tisa
Created by james mjema
No;0762940960
Kusali novena hii unaanza nia wimbo/nyimbo kisha unasali sala ya kila
siku na kumalizia na litania na Atukuzwe Baba….x3 kwa siku zote tisa.
BAADHI YA NYIMBO KWA
ROHO MTAKATIFU
NJOO WANGU MFARIJI
/Njoo wangu Mfariji
Yako shusha mapaji
Roho Mungu njoo/
Yako shusha mapaji
Roho Mungu njoo/
1.
Hekima nishushie, Mungu nimfuatie,
Roho Mungu njoo
2.
Akili nijalie, imani nizidie, Roho
Mungu njoo
3.
Nieneze shauri, imani nizidie, Roho
Mungu njoo
4.
Nizidishie nguvu, nsifanye ulegevu,
Roho Mungu njoo
5.
Elimu nieleze, hakika niongoze, Roho
Mungu njoo
6.
Ibada niwashie, Peke nikupupie, Roho
Mungu njoo
7.
Uchaji nitilie, dhambi nizichukie,
Roho Mungu njoo.
NJOO ROHO MTAKATIFU
/Njoo Roho Mtakatifu, shusha mapaji (kweli) niwe imara
x2
Leta nuru ya mwanga wako, ifikie moyoni mwangu x2/
Leta nuru ya mwanga wako, ifikie moyoni mwangu x2/
1. Roho mwenye
hekima, Roho wa shauri na nguvu
2. Nipatie elimu nitambue nafsi yako
3. Nipatie ibada nikusifu daima milele
4. Roho mwenye uchaji washa moto wako wa mapendo
2. Nipatie elimu nitambue nafsi yako
3. Nipatie ibada nikusifu daima milele
4. Roho mwenye uchaji washa moto wako wa mapendo
UJE ROHO (SEKWENSIA)
1. Uje Roho Mtakatifu, tuangaze toka mbingu, roho zetu
kwa mwangao
2. Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji, uje mwanga wa
mioyo
3. Ee Mfariji mwema sana, ee Rafiki Mwanana, ewe raha
mustarehe
4. Kwenye kazi u
pumziko, kwenye joto burudisho, u mfutaji wa machozi
5. Ewe mwanga wenye heri, uwajaze waumini, neema yako
mioyoni
6. Bila nguvu yako Wewe, mwanadamu hana kitu, kwake yote
yanakosa
7. Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu, na kuponya
majeraha
8. Ulegeze ukaidi, pasha moto ubaridi, nyosha upotovu
wote
9. Wape waamini wako, wenye tumaini kwako, paji zako zote
saba
10. Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila hila, wape heri
ya milele.
11. Amina aleluya, amina aleluya, amina aleluya.
11. Amina aleluya, amina aleluya, amina aleluya.
NJOO ROHO MTAKATIFU
1. Njoo Roho Mtakatifu, angalia zetu nyoyo, waletee neema
nguvu, wakosefu viumbevyo.
2. Majina yako Mfariji, shina la uzima pendo, wake
Mwenyezi upaji, mafuta ya roho moto
3. Ndiwe mnye mapaji saba, wa Mungu kuume mkono, mshika
uhadi wa Baba, mtoa kwa ndimi maneno
4. Angalo litung’arie, moyo kwa pendo tushushe, nguvu
neema tujalie, wanyonge wasabilitishe
5. Shetani mbali mkimbize, amani utupatie, tukufuate
tuongoze, maovu utukingie
6. Baba Mungu tujulishe, pia Mwana tumkubali, Roho
tukuungamie, mtokea wao wawili.
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA KWANZA, IJUMAA
ROHO MTAKATIFU ANATUFARIJI
Yesu alipokuwa
akiagana na mitume wake, kabla ya kupaa mbinguni, aliwaambia wasiondoke
Yerusalemu mpaka hapo watakapokuwa wamempokea Roho Mtakatifu. Aliwaambia:
“Wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni, mtajazwa nguvu, nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika nchi yote ya Yuda na Samaria, hata
kwenye mipaka yote ya dunia.” (Mdo.1:8)
Waliendelea kusali
pamoja toka hapo Yesu alipopaa mbinguni mpaka siku ya Pentekoste. Waliomba Roho
Mtakatifu awashukie, awajaze na mapaji yake. Na baada ya siku tisa Roho
Mtakatifu aliwashukia hao kundi dogo nao wakawa chanzo cha Kanisa lililopata
kuenea duniani kote.
Siku hizo tisa za
kusali zinaitwa NOVENA; na kila mwaka wakati huu, wakristu wakifuata mfano wa
mitume, wanasali muda wa siku tisa kabla ya Sikukuu ya Pentekoste. Wanamuomba
Roho Mtakatifu awashukie, awajaze nguvu na wingi wa mapaji yake.
Wakati huu wa
NOVENA , Tunayo mengi ya kuliombea Kanisa na kujiombea sisi wenyewe. Kwa hiyo
tumuombe Roho Mtakatifu atusaidie kusali vema na kuomba yale yote tunayohitaji
kwa maslahi yetu ya roho na mwili.
Na kama mtume
Paulo alivyowaambia wale waKristu wa kwanza, Roho Mtakatifu huja kutufatiji
katika udhaifu wetu. Basi tumuombe atufariji kwa sala hizi za NOVENA,
Atuwezeshe kusali na kuomba inavyotupasa kusali.
1. Ee Baba wa milele, tunakuomba umtume Roho Mtakatifu
atushukie sisi taifa lako awashe ndani yetu moto wa upendo wako.
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
2. Ee Baba mwema, tunakuomba utujalie faraja ya Roho
Mtakatifu sisi wana tulio katika dhiki na taabu nyingi mno hapa duniani.
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
3. Ulijalie Kanisa lako mapaji ya Roho wako Mtakatifu,
liweze kutekeleza vema utume wake wa kuhudumia watu wote hapa duniani.
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
4. Utujalie sisi kudumu katika NOVENA hii mpaka mwisho
kama Maria na mitume walivyodumu pamoja wakisali kabla ya Pentekoste ile ya
kwanza.
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
5. Utujalie neema zote zinazohitajika ili tuweze
kumshuhudia Kristu popote kwa mwenendo na matendo yetu ya kila siku,
tukiongozwa na Roho Mtakatifu.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
6. Uzijalie familia zote za wakristu neema na nguvu za
Roho Mtakatifu tupate kuendelea pasipo kuchoka katika sala na katika matendo
mema siku zote.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
7. Ewe Roho Mtakatifu, uwajalie vijana wetu moyo wa
ujasiri, wapate kulijenga kanisa lako na kueneza utawala wako katika jumuia
zetu za Kikristu.
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
TUOMBE;
Ee Mungu, uliye
muumba wa vitu vyote , tunakuomba utusikilize kwa wema sala zetu sisi taifa
lako, utuongoze sote tufuate siku zote utaratibu wa mapenzi yako; naye Roho
Mtakatifu atutegemeze mpaka mwisho wa novena hii. Tunaomba hayo kwa njia ya
Kristu Bwana wetu .
W. Amina.
W. Amina.
LITANIA YA ROHO MTAKATIFU
Bwana Utuhurumie………Utuhurumie
Kristu utuhurumie……..….Utuhurumie
Bwana utuhurumie….. Utuhurumie
Baba mweza wa vyote….. Utuhurumie
Yesu Mwana wa Pekee wa Baba na Mwokozi wa Dunia……..Utuokoe
Roho wa Baba na Mwana aunganishaye maisha ndani ya Baba na
Mwana………….Ututakatifuze
Roho Mtakatifu……….Utusikie
Roho Mtakatifu atokaye kwa Baba na Mwana…………..Njoo ndani ya mioyo yetu
Ahadi ya Mungu Baba……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Mionzi ya Mwanga kutoka Mbinguni……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Mwandishi wa vyote vilivyo vizuri……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Chanzo cha Maji ya Uzima……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Moto utumikao daima……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Muungano Mtakatifu……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Roho wa ukweli na upendo……………………Utuhurumie
Roho wa hekima na elimu……………………Utuhurumie
Roho wa shauri na nguvu……………………Utuhurumie
Roho wa akili na neema ya kumtumikia Mungu……………………Utuhurumie
Roho wa neema na sala……………………Utuhurumie
Roho wa amani na subira……………………Utuhurumie
Roho wa usafi na uaminifu……………………Utuhurumie
Kitulizo cha Roho……………………Utuhurumie
Roho aletaye Utakatifu……………………Utuhurumie
Roho uongozaye Kanisa……………………Utuhurumie
Zawadi kutoka kwa Mungu juu Mbinguni……………………Utuhurumie
Roho ajazaye ulimwengu……………………Utuhurumie
Roho Mtakatifu…………………..tupe neema ya kuchukia dhambi
Roho Mtakatifu…………………..njoo ufanye upya sura ya ulimwengu
Roho Mtakatifu…………………..jaza roho zetu kwa mwanga wako
Roho Mtakatifu…………………..ifuraishe mioyo yetu kwa sheria yako
Roho Mtakatifu…………………..washa moto wa mapendo ndani yetu
Roho Mtakatifu…………………..jaza mioyo yetu na hazina ya neema yako
Roho Mtakatifu…………………..tufundishe kusali vyema
Roho Mtakatifu…………………..tuangaze kwa nguvu zako za Ki-Mungu zitupatiazo
moyo wa kutenda daima yaliyo mema
Roho Mtakatifu…………………..tuongoze Kwenye njia ya wokovu
Roho Mtakatifu…………………..tuweze kufahamu yale ya muhimu tu
Roho Mtakatifu…………………..tupe hamu ya kuitafuta fadhila yako
Roho Mtakatifu…………………..tusaidie tuweze Kupata fadhila zote
Roho Mtakatifu…………………..tupe uvumilivu tuweze kutenda yaliyo mema tu.
Roho Mtakatifu…………………..tunaomba uwe zawadi ya uzima wetu
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za
dunia…………….Tushushie Roho wako Mtakatifu
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za
dunia…………….jaza mioyo yetu kwa mapaji yako ya Roho Mtakatifu
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za
dunia…………….tupe roho ya hekima na neema ya kumsifu Mungu.
Njoo Roho Mtakatifu uzijaze roho za waumini wako uwashe moto wa mapendo
yako ndani ya mioyo yetu
TUOMBE
Ee Mungu Baba mwenye
huruma tujalie Roho wako alete Mwanga kwetu ili apate kututakasa na kuingiza
ndani ya mioyo yetu Baraka za kuweza kutenda yale yaliyo mema.
Tunaomba hayo kupitia kwa Mwanao Mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo, anbaye anaishi na kutawala pamoja nawe katika Umoja wa Roho Mtakatifu. AMINA
Tunaomba hayo kupitia kwa Mwanao Mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo, anbaye anaishi na kutawala pamoja nawe katika Umoja wa Roho Mtakatifu. AMINA
Atukuzwe Baba…..x3
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA PILI, JUMAMOSI
ROHO MTAKATIFU ANATUSAIDIA KUENEZA INJILI
“Kweli nakwambia,
mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika utawala wa
Mungu,” (Yn. 3:5).
Kanisa limepewa na
Yesu ujumbe wa kuwaletea watu wote uzima mpya, uzima wa Mungu. Yesu aliwaambia
mitume wake: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Nendeni basi
mkawafanye watu wa makabila yote kuwa wafuasi wangu. Wabatizeni kwa Jina la
Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kuyashika maagizo yote
niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote mpaka mwisho wa nyakati (Mt.28:
18-20).
Sisi tuliobatizwa
tumepata kuwa viungo vilivyo hai vya Mwili wa Fumbo wa Kristu; kwa Kipaimara
tumeimarishwa na kuthibitishwa na Roho Mtakatifu. Tumekuwa taifa teule.
Tumeshirikishwa ule ukuhani wa Kristu. Tumepokea ujumbe wa kueneza utawala wa
Mungu.
Tunapopokea Sakramenti, na hasa ile Sakmenti ya Ekaristi, tunalisha imani na kuongeza mapendo, ambayo ni msingi wa utume wowote ule. Mapendo yanatuhimiza kueneza utawala wa Mungu na kumpenda Yesu Kristu aliyekuja kuwakomboa wanadamu wote.
Tunapopokea Sakramenti, na hasa ile Sakmenti ya Ekaristi, tunalisha imani na kuongeza mapendo, ambayo ni msingi wa utume wowote ule. Mapendo yanatuhimiza kueneza utawala wa Mungu na kumpenda Yesu Kristu aliyekuja kuwakomboa wanadamu wote.
Kila aliyebatizwa
anao wajibu wa kueneza imani ya Mungu na utawala wake. Kwa hiyo tumuombe Roho
Mtakatifu atuwezeshe kutimiza wito huo.
1. Ee Baba wa mbinguni
tunakuomba umpeleke Roho Mtakatifu aliangaze kanisa na kuliongoza, liweze
kuwafikishia mataifa yote habari njema ya wokovu.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
2. Ee Yesu Mkombozi wetu, umtume Roho Mtakatifu
awahimize wakristu wapate kutimiza wajibu wao wa kueneza neno lako popote
duniani
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
3. Ewe Roho Mtakatifu Mfariji, uamshe katika mioyo ya
vijana wengi hamu ya kupenda kulitumikia kanisa lako na kulihudumia taifa lako
kwa uaminifu.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
4. Ewe mwanga wa mataifa , uwajalie wanafunzi wasikie
sauti yako mioyoni mwao, nawe unapowaita wasikose kuisikia sauti yako, wawe
tayari kujitoa kwa ajili ya ndugu zao.
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
5. Uwasaidie wazazi wawalee vema watoto wao; uwatie
moyo katika wito wao, wapate pia kuishiriki vema ile kazi ya kueneza neno lako
kwa jirani zao.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
6. Ewe Roho Mtakatifu, uwasaidie wakristu wote kueneza
habari njema ya wokovu, kwa sala, kwa sadaka na kwa mifano ya maisha yao ya
uchaji.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
7. Ewe mpaji wa mema, uwajalie waumini mapaji yako
saba, wasichoke kulieneza neno lako kwa hekima pasipo hofu.
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
TUOMBE;
Ee Mungu, unapenda
watu wote waokoke, waifikie kweli yako. Tunakuomba uwapeleke wafanyakazi walio
wengi na wema katika shamba lako. Uwajalie kulihubiri neno lako kwa imani kuu
ili neno lako lienee na kupokewa na mataifa yote, wapate nao kukujua wewe peke
yako Mungu wao, Mungu wa kweli. Tunaomba hayo kwa nguvu ya Roho Mtakatifu
anayeliongoza kanisa lako sasa na milele.
W. Amina
W. Amina
LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo juu)
Atukuzwe Baba…..x3
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TATU, JUMAPILI
ROHO MTAKATIFU ANATUFANYA KUWA MITUME
Bwana
alisema kwa kinywa cha nabii Yoeli; “Katika siku zile za mwisho asema Bwana,
nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, waume kwa wake,
watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota
ndoto….hata watumishi wenu watamiminiwa Roho wangu katika siku zile, nao
watautangaza ujumbe wangu. (Mdo.2:17-21)
Siku
ile ya Pentekoste, bada ya Roho Mtakatifu kulishukia kanisa, mitume
waliwakumbusha watu maneno haya ya nabii Yoeli, na miaka mingi baadae, Petro
aliwaandikia barua Wakristu wa kwanza akawaambia; kila mmoja anapaswa kutumia
kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine, kama vile wakili mwema wa
zawadi mbali mbali za Mungu. Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya
Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu aliyojaliwa na Mungu ili
katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristu, ambaye utukufu na
nguvu ni vyake milele na milele (Pet 4;10-11).
Mtaguso
wa Pili wa Vatikano ulitukumbusha jambo hilo hilo uliposema; “Roho Mtakatifu
anayetakasa taifa la Mungu kwa njia ya Sakramenti amewapa waumini mapaji ya
pekee na kumjalia kila mmoja kadiri apendavyo. Kwa hiyo kila mmoja amgawie
mwenzake kadiri ya vipawa alivyopewa, awe mgawaji mwaminifu wa neema ya Mungu,
alijenge kanisa zima katika upendo.
Tunao
wajibu wa kutumia vipawa tulivyojaliwa na Roho Mtakatifu kwa manufaa ya kanisa
zima, na kwa faida ya watu wote. Tuunganike sote pamoja na wachungaji wote
katika kazi hiyo ya utume. Tumuombe basi Roho Mtakatifu atusaidie kutumia vema
vipawa vyake alivyotujalia.
1. Ewe Roho Mtakatifu uwape wakristu neema
na nguvu za kutumia vema vipaji ulivyowajalia kwa ajili ya kujenga kanisa lako
popote duniani, kwa ajili ya wokovu wa watu wote
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
2. Utujalie sisi sote mapaji yako saba,
tupate kukutumikia kwa uchaji
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
3. Utujalie tuwe mitume wa kweli wa
wenzetu, tushirikiane na wachungaji wetu katika huduma za kuwaongoza watu wote
na kuwafikisha mbinguni
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
4. Utujalie hekima na nguvu za kuwahudumia
watu wote kwa mapendo ya kweli yasiyo na kinyume
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
5. Utujalie neema ya kumpenda Mungu kwa
moyo wote na kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
6. Utupe neema ya kulisikia neno lako na
kulifuata, nayo mawazo yetu na matendo yetu yafuate daima mwongozo wako
mtakatifu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
7. Uwazidishie mapaji yako wale wote
wanaotumia vyema vipawa vyao, uwarudishe na wale wanaotumia vibaya rehema zako
W. Twakuomba utusikie
TUOMBE;
Ewe Roho Mungu ndiwe uliyewapa waumini vipawa vyako kwa kadiri unavyotaka. Utujalie tuyapokee na kuyatumia vyema mapaji yako mengi kwa ajili ya utukufu wa Jina lako na kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
W. Amina
Ewe Roho Mungu ndiwe uliyewapa waumini vipawa vyako kwa kadiri unavyotaka. Utujalie tuyapokee na kuyatumia vyema mapaji yako mengi kwa ajili ya utukufu wa Jina lako na kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
W. Amina
Litania ya Roho Mtakatifu …. (soma hapo juu)
Atukuzwe Baba…..x3
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA NNE, JUMATATU
ROHO MTAKATIFU ANALIUNGANISHA KANISA
“Atakapokuja huyu
Roho wa kweli , atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yn 16:13)
Baada ya kusema hayo,
Yesu aliinua macho yake kuelekea mbinguni akasema “Mimi nimekutukuza hapa
duniani; nimeikamilisha kazi uliyonipa niifanye. Naomba ili wote wawe kitu
kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba Wewe ulinituma (Yn 17:4,21).
Nasi twamuomba
Mungu Mwenyezi alijalie kanisa lake umoja wa kweli, awaunganishe wakristu wa
madhehebu yote katika zizi moja chini ya mchungaji mmoja.
Popote duniani
watu wengi, makundi kwa makundi wanavutwa na neema hiyo ya kuungana na kuufikia
umoja wa Kanisa. Hata ndugu zetu waliotengana nasi wanazidi kukubali mwongozo
wa Roho Mtakatifu na kutaka kurudi katika nyumba ya Baba na kuwa kundi moja
chini ya mchungaji mmoja. Isitoshe, hata sasa tena twaweza kuona kwamba kwa
namna fulani wamejiunga nasi katika Roho Mtakatifu, naye Roho Mtakatifu
anafanya kazi ndani yao kumshuhudia hata kwa kumwaga damu yao.Tena katika hao
ndugu zetu waliojitenga, Roho Mtakatifu analisha katika mioyo yao ile ya imani
inayowaunganisha wafuasi wote wa Kristu. Tumwombe basi Mwenyezi Mungu atujalie
hima huo umoja wa Kanisa lake tunaouania mno.
1. Ee Yesu Bwana wetu wewe umetuombea kwa Mungu Baba
tuwe itu kimoja kama Wewe ulivyo kitu kimoja na Baba. Utujalie huo umoja, ili
ulimwengu uone na kukiri kwamba ndiwe Bwana na Mkombozi wa watu wote
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
2. Ee Yesu utujalie moyo wa kulishika neno lako kwa
uaminifu, wala usituache kufuata njia zetu sisi wenyewe na kufarakana.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
3. Ee Yesu uliye Mchungaji wetu mwema, ondoa ndani
yetu ile tabia ya utengano, tupate kuwa sote kundi moja chini yako wewe uliye
mchungaji wetu mmoja.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
4. Ee Yesu, uliye Mchungaji mkuu, uwajalie wachungaji
wetu wawe siku zote na upendo wa Jina lako, wasichoke kulichunga vema kundi
lako hapa duniani na kuliweka pamoja lisitengane
W. Twakuombaa utusikie
W. Twakuombaa utusikie
5. Ewe Roho Mtakatifu, uziangaze akili za watu wote,
wapende siku zote kuishi kwa amani, umoja na mapendano
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
6. Ee Mungu, utufungulie …… wa muungano wako wa kweli
sisi tulio ndugu katika Bwana wetu Yesu Kristu.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
7. Utujalie mapatano na amani, tudumu tumeungana
katika familia zetu, katika jimbo letu na katika nchi yetu yote.
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
TUOMBE;
Ee Mungu,
utuunganishe sisi kondoo wako tuliotawanyika, tuwe chini ya Mwanao mpenzi,
tupate sote kuushiriki ule utawala wako wa kweli na haki, utawala wa neema na
amani, utawala wa upendo wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu W.
Amina
LITANIA YA ROHO MTAKATIFU …. (soma hapo juu)
Atukuzwe Baba…..x3
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TANO, JUMANNE
ROHO MTAKATIFU ANAWATAKASA WAUMINI
Walio wa Mungu
watafuata yaliyo ya Mungu, na walio wa dunia hufuata yaliyo ya dunia,. Ni mauti
kutosheka na mambo yaliyo ya dunia. Uzima na faraja ya kweli hupatikana tu
katika mambo ya Mungu.
Kwa nguvu zetu
sisi wenyewe hatuwezi kutenda lolote jema. Kuweza kwetu kwatoka kwa Mungu,
kwatoka kwa Yeye anayetupa kujua, kupenda na kutenda.
Mtu anapotenda
dhambi, hawezi kuongoka ila kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ndiye anayempa
mkosefu neema ya kutambua ubaya wa kosa lakena kuamua kuliacha. Ndiye anayempa
pia mkosefu kutambua uzuri wa neema aliyoipoteza na kumrudishia neema hiyo.
Ndiye anayempa nguvu za kuidumisha neema hiyo na kuiongeza.
Isitoshe, Roho
Mtakatifu ndiye anayemuwezesha mtu kuwa na maendeleo katika fadhila na utakatifu.
Ndiye anayemjalia imani iliyo msingi wa maisha ya kiKristu. Ndie anayetujalia
akili ya kushika mafumbo ya dini yetu na kuishi imani yetu mpaka kufa.
Lakini imani peke
yake haimtoshi mtu aokoke. Imani pasipo matendo haifai kitu; imani bila matendo
imekufa (Yak 2:28) Roho Mtakatifu anamuwezesha mtu kumuamini Mungu na kumenda
kuliko vitu vyote na kumpenda jirani kama kujipenda mwenyewe. Ndiyo maana Roho
Mtakatifu huitwa chanzo cha matendo yetu yote yaliyo mema. Basi, tumuombe Roho
Mtakatifu aitakase mioyo yetu sisi waumini wake, atuzidishie imani, atuwezeshe
kutenda matendo yaliyojaa imani.
1. Ewe Roho Mtakatifu, utudumishie imani, uyatakase
mawazo ya mioyo yetu yafuate daima maongozi yako na amri zako
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
2. Uzigeuze nia zetu zipate kumuelekea daima Mungu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
3. Utuwezeshe kuelekea katika utakatifu na kutenda
mema kwa imani siku zote za maisha yetu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
4. Utuzidishie imani matumaini na mapendo, tuweze
kushika kwa moyo thabiti yale yote tunayofundishwa na kanisa lako takatifu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
5. Uiwashe mioyo yetu na moto wa mapendo yako, tupate
kumpenda Mungu kweli na kumpenda jirani yetu pasipo unafiki.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
6. Utusaidie tuishi vema kwa imani na matumaini siku
zote za maisha yetu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
7. Utujalie kudumisha mioyoni mwetu ile neema ya
utakaso tuliyoipata mwanzo katika ubatizo wetu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
TUOMBE; Ee Mungu, mbele yako mioyo yetu i wazi; wewe wayajua
yote, wala hakuna siri iliyofichika mbele yako. Uyatakase mawazo ya mioyo yetu
kwa kutupelekea Roho Mtakatifu, ili tuweze kukupenda na kukutukuza kama
inavyostahili. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu W. Amina
LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo juu)
Atukuzwe Baba…..x3
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA SITA, JUMATANO
ROHO MTAKATIFU ANATUPA NGUVU
“Nitamuomba Baba ,
naye atawapelekea Mfariji mwingine atakaye kaa nanyi siku zote”. Katika maisha
yenu hapa duniani tunahitaji mno kitulizo cha Mungu. Ni jambo la hekima
kutafuta kitulizo hicho kwa Mungu wala si kwa viumbe; maana kitulizo
kinachopatikana kwa viumbe hapa duniani hakidumu; bali kitulizo kitokacho kwa
Mungu ni cha kudumu.
Roho Mtakatifu
ndio kitulizo chetu cha kweli. Baba ndiye aliyetuumba, Mwana ndiye
aliyetukomboa, Roho Mtakatifu ndiye aliyetutakasa mioyo yetu na kutufariji.
Kazi ya Roho
Mtakatifu sio tu kuwatuliza wale walio na huzuni, bali pia kuwapa moyo wa
kuvumilia taabu zozote kwa saburi.
Tunahitaji nguvu
ya Roho Mtakatifu ili tuweze kuishi maisha mema ya kikristu. Katika juhudi zetu
za kumtumikia Mungu mara nyingi tunakutana na shida; naye Roho Mtakatifu ndie
anayetufariji kwa kutupa nguvu za kupambana na matatizo yote. Maisha yetu hapa
duniani yamejaa misalaba. Na misalaba hiyo hatuwezi kuichukua kwa nguvu zetu
wenyewe. Roho Mtakatifu ndie anayetupa nguvu za kuvumilia. Basi, tumuombe aje
kutufariji na kutupa nguvu za kuchukua msalaba wetu kwa saburi kila siku.
1. Ee Yesu Bwana wetu, tunakusihi Wewe na Baba mumtume
Roho Mtakatifu atufariji, awajalie kitulizo wale wote walio katika taabu na majonzi
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
2. Ewe Roho Mtakatifu, uwafariji wale walio katika
tabu za namna zozote ili waweze kuvumilia kwa saburi mateso yao kwa faida ya
Roho zao na roho za ndugu zao.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
3. Uwafariji wale walio wagonjwa, uwajalie afya ya
roho na ya mwili
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
4. Uwasaidie yatima, wajane na wote walioachwa,
wasikose kupata siku kwa siku mahitaji yao ya lazima
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
5. Wajalie wale wote walio walegevu na wakosefu neema
ya kuongoka na kurejea hima katika amani ya upendo wako
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
6. Uwaimarishe wale walio wema, uwajalie neema ya
kudumu wasilegee katika kutenda mema leo na kesho na siku zote za maisha yao.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
7. Utujalie nguvu za kutafuta na kudumisha amani ya
kweli katika mioyo yetu na kati ya ndugu zetu katika jumuia zetu za kikristu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
TUOMBE;
Ee Bwana Mungu
wetu, tunakuomba neema ya Roho Mtakatifu ituangaze akili na mioyo yetu na
kutujaza nguvu ya upendo wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
W. Amina
LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo juu)
Atukuzwe Baba…..x3
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA SABA, ALHAMISI
ROHO MTAKATIFU ANATUPA HEKIMA
Hekima tunayopewa
na Roho Mtakatifu si sawa kama hekima inayopatikana katika ulimwengu huu.
Hekima ya Roho
Mtakatifu ni ile Mtk. Paulo aliyowaambia Wakorintho ya kuwa; ni hekima ambayo
watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana kama wangaliielewa,
hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu. Lakini, ni kama yasemavyo maandiko; mambo
ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio kuyasikia mambo ambayo binadamu
hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao
(1Kor 2;8-9).
Mtk. Paulo alisema
kama vile roho ya mtu ndiyo yenye kufahamu na kutambua yaliyo ndani yake; hivyo
pia Roho Mtakatifu ndiye anayefahamu mambo ya Mungu na kutufumbulia sisi
mioyoni mwetu.
Katika Sikukuu hii
ya Pentekoste tunatazamia kumpokea Roho Mtakatifu. Yeye aliye hekima ya Mungu
atatufumbulia siri za Mungu na ukweli wake. Ndiye atakayeamsha ndani yetu
mapendo ya Yesu Msulibiwa , Mkombozi wetu. Ni yeye atakayetuongoza kutenda mema
na kuacha mabaya; tunahitaji sana Roho Mtakatifu katika maisha yetu ya kila
siku, tupate hekima ya kuchagua na kutenda daima yaliyo mema. Katika novena hii
tuzidi kumuomba Mungu atushushie Roho Mtakatifu, atujaze na hekima yake.
1. Ee Mungu, uwabariki viongozi wa dini na wasaidizi
wao, wapate kutuongoza kwa hekima na mapendo
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
2. Ewe Roho Mtakatifu, utujalie hekima ya kutambua
Mambo ya Mungu na kuyatekeleza kwa uchaji
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
3. Utujalie kuyajua mapenzi ya Mungu na kuyapokea kwa
furaha
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
4. Uamshe ndani yetu mapendo ya Yesu msulibiwa ,
utuwezeshe kutimiza vema wajibu wetu kama wafuasi wa kweli wa Kristu Bwana wetu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
5. Utuwezeshe kuchagua daima yaliyo mema na
kuyatekeleza, tupate kulijenga na kulidumisha kanisa lako hapa duniani
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
6. Utuepushe na mafundisho yoyote yaliyo na upotovu,
utujalie hekima ya kuzidi kutambua ukweli wako na mafundisho yako yaletayo
wokovu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
7. Hekima ya Roho Mtakatifu ituongoze katika satfari
ya maisha yetu hapa duniani, tupate mwishowe kukurudi Wewe Muumba wetu uliye
mwanzo wetu na mwisho wetu
W. Twakuomba utusiki
W. Twakuomba utusiki
TUOMBE;
Ee Mungu, Baba wa
utukufu, tunakuomba utupe Roho wako wa hekima, atuwezeshe kukufahamu vema,
atuongoze kuishi maisha yenye kukupendeza. Utusaidie kupambana na matatizo ya
maisha, tupate kuishi maisha mema hapa duniani na mwisho tupate tunzo la heri
na furaha yako huko mbinguni. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu.W.
Amina.
LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo juu)
Atukuzwe Baba…..x3
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA NANE, IJUMAA
ROHO MTAKATIFU ANATUPA MWANGA.
Roho Mtakatifu
anaangaza akili zetu tuweze kuona ukweli wa Mungu na kuufata. Bila Roho
Mtakatifu akili zetu zimo katika giza nene, wala hatuwezi kuona njia ya
kutuelekeza kwa Mungu.
Mungu alipoumba
ulimwengu, dunia ilikuwa giza tupu, haina kitu. Mungu alisema; “Iwe nuru”,
ikawa nuru, Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema (Mwa 1;3-4) vivyo hivyo akili
ya binadamu bila nuru ya mwanga wa Roho Mtakatifu, ni tupu, ina giza, haiwezi
kuona mambo yanayotuelekeza kwa Mungu. Tukiwa na nuru ya Roho Mtakatifu tunaona
ukweli wa Mungu jinsi ulivyo.
Roho Mtakatifu
anapoijia roho ya mtu, anaiangaza akili yake iweze kuona mambo yanayofaa kwa
wokovu. Naye akiisha kuiangaza akili ya mtu huimarisha utashi wake na
kumwezesha kuchagua daima yaliyo mema.
Roho Mtakatifu
huiangaza akili iweze kuona ukweli. Kabla ya kuwaaga mitume, Yesu aliwaambia
kuwa atawapelekea mfariji mwingine atakayekaa nao siku zote. Roho wa kweli
ambaye dunia haiwezi kumpokea kwa sababu hawakumfahamu, lakini wao mitume
watamfahamu kwa maana atakaa nao siku zote. Yesu ametuahidi pia sisi Roho huyo
akae nasi
Leo hivi duniani kuna uwongo na udanganyifu mwingi; kuna dhuluma, vita, na maovu ya kila namna. Hii ni kwa sababu dunia haijamtambua bado Roho Mtakatifu na kumpokea Yeye aliye mwanga wa dunia na asili ya kweli yote.
Leo hivi duniani kuna uwongo na udanganyifu mwingi; kuna dhuluma, vita, na maovu ya kila namna. Hii ni kwa sababu dunia haijamtambua bado Roho Mtakatifu na kumpokea Yeye aliye mwanga wa dunia na asili ya kweli yote.
Mtaguso wa Pili wa
Vatikano watambua ya kuwa Roho Mtakatifu anakaa katika kanisa na katika mioyo
ya waumini kama katika hekalu. Roho Mtakatifu analiongoza kanisa na kulifanya
liwe na umoja; analipamba na mapaji yake mabalimbali.
Tumuombe Mungu
Baba ampeleke huyo Roho Mtakatifu katika kanisa lake, aliongoze na kulilinda
lisipate kutengana, bali lisaidie kueneza utawala wa Mungu popote duniani.
1. Ewe Roho Mtakatifu, utujalie kuona
mwanga wa kweli yako na kuifuata
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
2. Uwape waregevu neema ya kuirudia tena
njia ya kweli yako
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
3. Utuwezeshe sisi sote waamini wako
tutembee siku zote katika nuru ya kweli yako na sheria zako
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
4. Utuangazie akili ya mioyo yetu tuchague
daima yale yanayakupendeza
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
5. Uwape mwanga wako viongozi wetu wa dini
na serikali, wapate kutuongoza kwa hekima na uchaji, wasisahau kamwe kwamba
uwezo walionao unatoka kwa Mungu.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
6. Utupe mwanga wako tuwaone watu wote kama
ndugu zetu. Tuishi kindugu na kusaidiana kindugu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
7. Ewe Roho Mtakatifu ndiwe mpatanishi wa
mioyo,; tunakuomba uondoe udhalimu, uonevu, udanganyifu na maovu yote katika
mioyo ya watu wote.
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
TUOMBE;
Ee
Yesu Bwana wetu, uliyesema “Pasipo Mimi hamuwezi kitu” umpeleke Roho Mtakatifu
atuangaze akili zetu, tupate kufahamu mapenzi yako na kuyatimiza kwa imani na
uchaji. Roho Mtakatifu atuongoze katika mambo yote, yeye anayeishi na kutawala
nawe pamoja na Baba daima na milele.
W. Amina
LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo juu)
Atukuzwe Baba…..x3
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TISA, JUMAMOSI
ROHO MTAKATIFU ANATUPA MAPENDO
Maandiko
Matakatifu yanatuambia ya kuwa, Roho Mtakatifu, Nafsi ya Tatu ya Utatu
Mtakatifu, ndiye Upendo katika Baba na Mwana. Upendo hujieneza. Naye Roho
Mtakatifu aliye pendo lenyewe la Mungu, hupenda kujieneza na kujishirikisha
nasi, na kuwasha ndani yetu moto wa mapendo yake.
Roho Mtakatifu
ndiye mwenye kutakatifuza roho zetu kwa neema ya utakaso. Neema hiyo ni uzima
wa Mungu, ndio huo upendo wa Mungu tunaoshirikishwa. Roho isiyo na neema ya
utakaso imetengana na Mungu, haina uzima wake, haina upendo wake, kwa hiyo
haiwezi pia kuwa na mapendo ya kweli ya jirani.
Ingawa tunaona
ishara nyingi za watu kupendana kidugu hapa duniani, mapendo hayo si mapendo ya
kweli wala si kamili kama hayatokani na neema ya utakaso rohoni mwa mtu. Kama
hakuna neema ya utakaso ndani yetu, Mungu pia hayupo kati yetu.
Roho Mtakatifu
anatuunganisha na Mungu katika upendo. Pasipo na mapendo hapana mapatano, hapana
masikilizano wala mwungano. Watu wanaopendana wanaungana na kulingana katika
fikra zao na nia zao. Roho Mtakatifu anayetutia mapendo rohoni na kutuwashia
moto wa mapendo, ndiye anayetuwezesha kuwa na mawazo ya namna moja na nia moja.
Watu wanaopendana hupenda
kukaa pamoja, kuishi pamoja na kusaidiana. Roho Mtakatifu aliye chanzo cha
mapendo ya kweli hutuweka pamoja katika Kanisa lake. Hukaa ndani yetu, hukaa
katika Kanisa na kuwasha moto wa mapendo yake ndani yetu. Roho Mtakatifu
anatuwezesha kukaa kwa amani nyumbani, kazini na katika jumuiya zetu. Basi,
tumwombe sasa Roho Mtakatifu atuongezee hayo mapendo yake ndani yetu.
1. Ewe Roho Mtakatifu, uwashe mioyoni mwetu moto wa
mapendo yako, tupate kuwapenda jirani zetu kama tunavyotaka kupendwa nao.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
2. Udumishe ndani yetu neema hiyo ya mapendo yako,
tuwezeshe kuishi kwa amani leo na siku zote za maisha yetu.
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
3. Utujalie neema na nguvu za kutekeleza mema yote
tunayokusudia kuyatenda siku hii ya leo
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
4. Uongoze nia zetu na maazimio yetu, yalingane na
juhudi zetu za kutaka kuleta mafanikio ya roho na mwili kati yetu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
5. Utubariki, ili baada ya maombi haya, tuwe na juhudi
ya kutimiza vema zaidi wajibu wetu wa kikristu kwa moyo mkuu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
6. Utuwezeshe kueneza mapendo na amani kati yetu na
katika jumuiya zetu za kikristu
W. Twakuomba utusikie
W. Twakuomba utusikie
7. Utuwezeshe kuwa kweli chachu ya wema na mapendano
kati ya watu, ili nao wapate rehema zako kwa maombezi yetu.
W. Twakuomba utusikie.
W. Twakuomba utusikie.
TUOMBE;
Ee Mungu,
tunakushukuru kwa neema ulizotujalia, hata tukaweza kuifanya ibada hii ya
Novena takatifu mpaka mwisho. Utujalie mema yote tuliyoomba; utusaidie
kutekeleza yote yale tuliyokusudia kutenda. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu
Bwana wetu.
W. Amina.
LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo juu)
Atukuzwe Baba…..x3
Created by james mjema
No; 0762940960